Monday, July 30, 2012

Wanafunzi katika miji ya Tunduma na Vwawa wilayani Mbozi wameandamana hadi ofisi za halmashauri wakidai haki zao. Wanafunzi hao walielezwa sababu ya hali hiyo na kuwafanya wanafunzi kutoridhika na ndipo walipojilaza barabarani kuzuia magari yasipiti hali iliyochochewa na baadhi ya wananchi na hivyo kuwalazimu polisi kuwatawanya kwa mabomu ya machozi. Ofisi ya halmashauri ya mji wa Tunduma zimevunjwa na wanafunzi walioandamana. Aidha nyaraka muhimu zote za ofisi hizo zimechukuliwa na kutawanywa ovyo barabarani, pikipiki moja imechomwa moto, computer ya ofisi imeibiwa. Wanafunzi wa shule za Halori na Ichenjezya mjini Vwawa walizuiwa katika lango kuu la halmashauri (Gate) ambapo polisi walifauru kuwaondoa kwa kuwabembeleza. wanafunzi hao walipohojiwa na mwandishi wa habari hii walidai kuwa walimu wao wamegoma na kuwanyima haki ya kusoma ambayo ndiyo wanayoidai. hata hivyo ofisi za Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri zilifikwa na wakati mgumu hadi kusababisha shughuli nyingine kusimama kwa muda.

Site search

    More Text