Alishikiliwa kwa masaa matatu, hakunywa maji japo alizamishwa kwa masaa hayo, maajabu hayo!
Unaweza kuona makovu makubwa mikononi mwake hapa ni baada ya kutoka katika hospitali ya Peramiho
“Mungu
asiporuhusu kufa huwezi kufa hadi aruhusu yeye” ndivyo anavyoanza kusimulia
kisa cha kusisimua na cha ajabu Erika Kajuanga (70) mwanamke aliyenusurika
kuliwa na mamba baada ya kushikiliwa kwa masaa matatu chini ya maji.
Erika
Kajuanga ni mkazi wa kijiji cha Bujonde wilayani Kyela mkoa wa Mbeya ambaye
alifikwa na mkasa wa kukamatwa na mamba mnamo Novemba 27 mwaka 2012 majira ya
saa moja asubuhi alipokuwa anafua nguo kando ya mto Kiwira.
“Nikiwa
nafua nguo ghafla nilishikwa na mamba ambaye alinizamisha kwenye maji akikimbia
toka pale aliponikamatia na kunipeleka ndani zaidi umbali ambao wenzagu
tuliokuwa tunafua nao hawakuweza kubaini”anasimulia.
Akiwa huko
chini mamba alimwingiza kwenye pango chini ya maji akiwa tayari amemvunja
mikono yote miwili na kumjeruhi goti na kumuacha kwa muda baadaye mamba huyo
alirejea na kumtoa pale alipomuacha na kumwinua juu na kisha kumzamisha tena.
Mama huyo
alikuwa akiomba Mungu amnusuru na hatari hiyo. Fahamu zilimjia akaingiza mdomoni
mwa mamba nguo aliyokuwa ameshikilia mkononi licha ya mikono hiyo kuvunjwa
aliweza kuishindilia vizuri kinywani mwa mamba huyo ndipo alipomwachia na
kukimbia.
Akiwa chini
ya pango kwenye maji mama huyo anashindwa kujua ilikuwaje hakudhuliwa na maji
kwani hadi anatoka hakunywa hata kidogo na kwamba aliwezaje kupumua kwenye maji
bado kwake ni kitendawili.
Baada ya
kuachiwa hakuwa na uwezo wa kuogelea hivyo alijilaza chali akitumia miguu
aliweza kufika eneo lenye jiwe kubwa akiwa hapo aliwaona watu waliokuwa
wanajitahidi kumtafuta akapiga ukulele wa kuomba msaada ndipo walipofika
wanaume wenye mikuki na kumwokoa.
Anasema
ilifika hatua alikata tamaa ya kuokoka kwani alijua mamba yule angeweza
kumrudia wakati wowote kabla hajapata msaada.
Alikimbizwa
katika hospitali ya Kyela na kupatiwa msaada kisha kukimbizwa katika hospitali
ya rufaa Mbeya ambapo hakuweza kupata matibabu yoyote kwasababu ya kutokuwa na
fedha. Aliambiwa atoe shilingi laki tatu. Hata hivyo Kajuanga anadai kuwa
yalitokea mabishano kati ya wahudumu wa hospitali hiyo waliodai kuwa bibi
amepona kifo cha mamba na sasa mnamwacha afie hospitali kwa kukosa matibabu.
Kama ilivyo
ada ya mja hunena mahali pande mbili zikivutana Mungu huinua upande mmoja
kumtetea mja wake, walijitokeza ndugu na kumsaidia kumpeleka katika hospitali
ya Peramiho iliyoko Songea mkoani Ruvuma baada ya kuwepo katika hospitali ya
rufaa Mbeya kwa siku tatu bila matibabu.
Erika Kajuanga anawashukuru watu wa Mungu
ambao walijitolea na kumsaidia kwenda katika hospitali ya Peramiho ambako
anaendelea na matibabu hadi leo na kwamba hali yake inaendelea vizuri baada ya
mikono iliyovunjwa kuungwa vizuri.
Tukio hili
liliwashangaza wanakijiji wa Bujonde wakijiuliza bibi huyo aliwezaje kuwa
mikononi mwa mamba kwa masaa matatu na baadaye kuachiwa; kweli Mungu mkubwa.
Unaweza kuona makovu makubwa mikononi mwake hapa ni baada ya kutoka katika hospitali ya Peramiho
0 comments:
Post a Comment
Thank you for reading the article