Wadaiwa
shilingi 50,000 kwa ajili ya maabara za shule ndipo maombi yafikiriwe
Serikali
inahusika na kuwacheleweshea wakulima pembejeo, kutokana na kushindwa
kukamilisha mikataba na wadau wa kilimo kwa wakati.
Hayo
yalielezwa jana na afisa kilimo wa mkoa wa Mbeya Enock Nyasebwa alipozungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alitoa
kauli hiyo kufuatia malalamiko ya wakulima wa wilaya za Mbozi na Momba ambao
kupitia vikundi vyao waliomba serikali mapema mwaka huu kuwakopesha pembejeo za
kilimo cha mahindi.
Maombi
hayo ya mikopo ya pembejeo yametokana na serikali kubadili mfumo wa kutoa
pembejeo kwa njia ya ruzuku ambao ulishindikana na kubuni mpango mpya ambao
wakulima kupitia vikundi vyao wanaomba mkopo kupitia idara ya kilimo na benki
na serikali kutoa mkopo huu ukiwa umechangiwa na wakulima kwa asilimia 20 na
riba ya mkopo kulipwa na serikali.
Hata
hivyo serikali imeonekana kusuasua katika kutekeleza mpango huo hali
iliyowasababishia wakulima kupata pembejeo kwa wakati muafaka.
Akizungumza
na gazeti hili mwenyekiti wa chama cha wakulima wa Momba Sadiki Simaya alisema
kuwa serikali iliahidi kutoa pembejeo kabla ya msimu wa kilimo kuanza lakini mpaka
sasa mvua zimeanza na hakuna lolote katika utekelezaji wa mpago huo.
Simaye
aliongeza kuwa kutokana na hali hii wana wasiwasi kuwa huenda wakashindwa
kupanda mahindi kwa wakati na hivyo kupata hasara na kuongezeka kwa gharama
kwani mashamba yaliyolimwa yameanza kuota nyasi na hivyo kuwalazimu kulima tena
waliwa wanasubiri pembejeo.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Halungu Charles Simkoko ameeleza kusikitishwa na mipango ya
serikali ya kuwatoza vikundi vya wakulima mchango wa shilingi 50,000 kwa ajili
ya ujenzi wa maabara kama sharti la kupata mikopo hiyo ya pembejeo.
Mkulima
mwingine kutoka Tunduma Economic Group Dr Samson Kibona alilalamikia utaratibu
huo kuwa unaweza kuwaathiri wasipate mazao ya kutosha msimu huu iwapo
watachelewa kupanda mazao yao kwa wakati kwani mvua za kwanza ni za kupandia.
Akifafanua
zaidi Kibona alisema kuwa mpaka sasa wameshindwa kuuza mahindi ya mwaka huu kwa
kukosa soko hali inayowafanya washindwe kufanya chochote zaidi ya kungojea
mikopo hiyo.
Hata
hivyo afisa kilimo huyo wa mkoa alitetea ucheleweshaji huo kuwa serikali
inafanya mazungumzo na wadau wa kilimo yakiwemo mabenki na makampuni ya ununuzi
wa mazao na kuhakikisha kuwa wakulima wanaingia mikataba kwa kutoa asilimia 20 ambapo
serikali itatoa asilimia 20 na mabenki kutoa asilimia 60 ya mkopo huo
“tunaamini kuwa wakulima watapata pembejeo mapema mara baada ya kukamilisha
mikataba hiyo” alisisitiza.
Naye
afisa kilimo wilaya ya Mbozi alipohojiwa juu ya kuweka masharti ya kuchangia
50,000 kwa vikundi vinavyoomba mkopo alisema sisi tunawaomba tu hatuwalazimishi
kauli inayopingwa na viongozi wa vikundi.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment
Thank you for reading the article