Saturday, September 27, 2008

WAFA WAKICHIMBUA VITO VYA WAJERUMANI

Posted by Unknown On 12:49 AM No comments
Mbozi September 27, 2008 VIFO

WATU watatu wamefariki wakifukua hazina inayodhaniwa kufukiwa na wamishionari Wajerumani katika kijiji cha Mbozi wilayani Mbozi mkoani Mbeya.

Tukio hilo lililotokea juzi mchana katika eneo la kanisa la Moravian usharika wa Mbozi Mission lilisababishwa na watu hao kukosa hewa katika shimo hilo ambalo linaaminiwa kufukiwa dhahabu na rupia.

Afisa Mtendaji kata ya Igamba Ambakisye Waya amewataja marehemu kuwa ni Green Sichone (50), mapacha Erick na Sadock Mnkondya (30) wote wakazi wa kijijini hapo.

Waya alisema kuwa mapema mwaka huu wachimbaji hao walipata taarifa kutoka kwa mtu asiyefahamika zikielezea kuwepo kwa hazina kubwa ya dhahabu, sarafu na vito mbalimbali vya thamani vilivyohifadhiwa na wamishenari wa Kijerumani waliofika kufungua misheni hiyo mwaka 1902.

“Agosti mwaka huu watu hao walituma maombi kwa baraza la wazee wa kanisa chini ya Mchungaji Lordrick Sichone ya kutaka kuchimbua eneo hilo na kutafiti iwapo haizna hiyo ipo, baraza liliwaruhusu kufanya kazi hiyo” Aliongeza mtendaji huyo.

Alisema kuwa watu hao walichimba mashimo mawili kati ya mwezi Agosti na Septemba ambapo katika shimo la pili lililokuwa na upana wa mita 2 na kina mita 17 walipata vikwazo kwa kuibuka maji na upungufu wa hewa ambapo iliwalazimu kutumia mashine ya kuvuta maji na kupeleka hewa.

Naye Mchungaji Sichone alisema kuwa baada ya kuona watu hao hawatokei kwa muda mrefu aliamua kwenda kuchungulia ambapo aliona shimo likiwa limejaa moshi na harufu ya petroli na maiti wakielea juu ya maji.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Zerothe Stephen alithibitisha tukio hilo na akamtaja Mchungaji Sichone kuwa ndiye aliyegundua tukio hilo.

Mwisho
km/

0 comments:

Post a Comment

Thank you for reading the article

Site search

    More Text