Katika ziara hiyo tuliweza kujionea jinsi maanguko ya ardhi (Land slide) yalivyathiri maeneo mbalimbali kabla ya kufika Matema.
Mgahawa mzuri unaofaa kwa mahitaji ya utalii ulitoa huduma safi kwa waandishi waliofika eneo hilo. Hii ni nafasi ya waandishi kutangaza utalii na kutambulisha umma kwa vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Mbeya.
Gari hilo lililopambwa vema liliendeshwa na dreva mwanamke lilitufikisha salama licha ya matatizo madogo madogo ya njiani.
Tulijionea samaki wanaovuliwa ziwa Nyasa. Ziwa lilionekana kuwa na upungufu mkubwa wa samaki ambao ilielezwa kuwa tatizo linatokana na uvuvi usiozingatia utaalam.
Ziwa hilo linatoa samaki wa mapambo (wenye rangi) na ambao wakivuliwa husafirishwa nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment
Thank you for reading the article