Sunday, August 29, 2010

WANAFUNZI WATALII

Posted by Unknown On 2:57 AM 2 comments
Ziara ya wanafunzi wa shule ya awali na msingi ya Uwata Mbeya katika picha
 
Mkuu wa kituo cha utafiti wa kahawa (Tacri) kituo cha Mbimba Mbozi Isack Mushi akitoa maelezo ya namna ya kuzalisha miche ya kahawa kwa njia za kisasa kwa wanafunzi wa Uwata Nursery and Primary School ya jijini Mbeya waliotembelea kituo hicho hivi karibuni.

wanafunzi hao wakitazama michoro ya kale iliyoko katika miamba katika kijiji cha Nkangamo wilayani Mbozi. Michoro hiyo inayokadiriwa kuwa ilichorwa miaka 3000 iliyopitwa ni sehemu muhimu kwa utalii na kuwa chanzo ya mapato ya serikali kupitia utalii. Kwa bahati mbaya idara husika imejifanya haioni na hivyo kutofika katika eneo hilo. Kama wadau hatukati tamaa tutaendelea kuwakumbusha hadi waamke katika usingizi, waanze kupatengeneza tayari kwa kutembelewa na watalii.



Huo nao ni mwamba katika eneo hilo, nitauza picha hizo zitumike kama wall paper kwenye komputa pengine naweza kupunguza umaskini wa kipato. Haijulikani vizazi vilivyoishi hapo vilikuwa na teknolojia ya jinsi gani kwani michoro yote hapo ipo katika miamba inayoning'inia (hanging rock) na wino uliotumika ni mwekundu. Profesa Jengo aliwahi kueleza katika warsha moja mwaka 2004 kuwa michoro hiyo mahali pote duniani wino wao ulikuwa ni rangi nyekundu isiyofutika kwa karne na karne.
Michoro hiyo haijatafsiriwa maana yake pengine ni kwasababu idara ya mambo ya kale haijui kama kuna michoro hiyo licha ya kuwataarifu hata kwa maandishi. Tunachoweza kusema ni kuwa maeneo waliyoishi jamii za wakulima zilichora michoro isiyoweza kutafsirika kwa lugha zetu tofauti na walikoishi jamii za wawindaji ambao walichora wanyama, mitego au mikuki na hivyo kutufikishia ujumbe kuwa wao waliishi kwa uwindaji.
  
Wanafunzi wakiangalia alama ya unyayo wa kiumbe kinachodhaniwa kuwa binadamu katika mwamba huo ambao wenyeji wa kijiji cha Nkangamo wanautumia kama jamvi la kuanikia mihogo, ulezi na mahindi kama unavyoweza kujionea


Hebu tuungane na watoto hawa kushangaa michoro hiyo

2 comments:

  1. nimepapenda hapa mahala, naomba details za kufika. ahsante, nitumie kwa saidmdee@hotmail.com

    ReplyDelete

Thank you for reading the article

Site search

    More Text