Na Kenneth Mwazembe
Tunduma
Msongamano wa magari makubwa ya mizigo yanayokwenda katika nchi za kusini mwa Afrika umeendelea kuwa kero kwa wakazi wa mji wa Tunduma wilayani Mbozi licha ya jitihada za serikali kwa kutumia askari wa usalama barabarani ambazo hazijasaidia chochote.
Wakazi wa mji huo (wameomba majina yao yahifadhiwe) wameitaka serikali kujenga maegesho nje ya mji haraka ili kuondoa kero linalowakabiri.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi Aden Mwakyonde alipotakiwa na mwandishi wa habari hizi kueleza kuhusu kero hiyo alisema kuwa serikali ina mpango wa kujenga maegesho yenye kuweza kupokea magari 2000 katika eneo la Chapwa mara watakapopata fedha.
Hali hii inatoa mwanya kwa wahalifu kufanya vitendo viovu kama mauaji, wizi na unyang'anyi kama ilivyotokea mwezi uliopita. ambapo watu wanaodhaniwa kuwa majambazi waliwaua watu wanne na kujeruhi wawili walipovamia majumba ya starehe .
0 comments:
Post a Comment
Thank you for reading the article