Home
Business
Internet
Market
Stock
Downloads
Dvd
Games
Software
Office
Parent Category
Child Category 1
Sub Child Category 1
Sub Child Category 2
Sub Child Category 3
Child Category 2
Child Category 3
Child Category 4
Featured
Health
Childcare
Doctors
Uncategorized
Thursday, February 14, 2008
WANAHABARI WANOLEWA
Posted by Unknown
On 12:15 PM
No comments
Na Kenneth Mwazembe, Mbeya
Februari 12, 2008
Wanahabari nchini wametakiwa kutumia taaluma zao bila woga kuisaidia serikali kwa kufichua maovu yanayofanyika nchini ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahili kwa jamii na hivyo kuifanya kutekeleza wajibu wake kwa wananchi.
Wito huo umetolewa jana na Makamu mwenyekiti wa MISA-Tanzania Jonas Mwasumbi wakati akifungua mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi kwa waandishi wa habari ya siku nne ya Uandishi habari za Uchunguzi katika Ukumbi wa Paladise Inn mjini Mbeya yanayofadhiliwa na Millenium Challenge Corporation (MCC)ya serikali ya Marekani kupitia shirika la misaada la USAID, ambayo wawezeshaji wake ni PACT Tanzania ikishirikiana na MISA.
Mwasumbi alisema kuwa elimu ya uandishi wa habari za uchunguzi utawawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi hivyo kupambana na vitendo vya kifisadi, hujuma, ubadhilifu na kila aina ya uozo uoingamamiza jamii inayohitaji
maendeleo.
Alisema habari za uchunguzi zinaifanya serikali kuwajibika vyema katika utekelezaji wa majukumu yake kwa wananchina kwamba mwandishi wa habari ni kioo, jicho, mdomo na sikio la jamii wakiwemo wanyonge.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye ni mshauri wa Magazeti ya Mwanahalisi, Ndimala Tegambwage alimewataka wanahabari kuwa makini, wabunifu na kuwa na shauku ya kuona na kujua zaidi ya vile mtu wa kawaida angeweza
kuona.
Tegambwage akifafanua juu ya uandishi wa habari chokonozi alisema mwandishi wa habari anatakiwa kuwa na jicho la ziada ili aweze kuona, kusikia na kusema yale aliyoyaona kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuwa sauti ya wanyonge na jicho la wasioona.
Naye mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Mbeya, Christopher Nyenyembe amewataka waandishi wa habari kwa kutumia mafunzo wanayoyapata kumsaidia Waziri mkuu, Bw. Mizengo Pinda na Baraza jipya la Mawaziri lililoteuliwa kupambana na maovu mbalimbali ikiwemo rushwa na ubadhirifu wa mali za Umma.
Nyenyembe alisema kuwa kwa kuwa Waziri mkuu huyo Mpya Pinda alikuwa mstari wa mbele kukemea matumizi mabaya ya fedha za halmashauri za wilaya, manispaa na miji hapa nchini atahitaji msaada wa waandishi katika kufichua maovu yanayofanyika katika halmashauri hizo.
Aidha washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru PACT Tanzania kwa kuandaa mafunzo ambayo yanawajengea uwezo wa kupambana na maovu kijasiri na kuwawezesha kubadilishana uzoefu wa kazi zao za kila siku miongoni mwao.
Wameiomba serikali kuona umuhimu wa kuvitumia vyombo vya habari bila kuangalia ni vya binafsi au vya serikali kwani vyote vinafanya kazi kwa lengo la kuisadia jamii.
Wakitoa mfano walisema kuwa kashfa ya Richmond ambayo imekuwa mzigo na donda ndugu kwa watanzania iliibuliwa na vyombo vya habari binafsi na baadaye ikathibitika kwa kupitia kamati iliyoundwa na Bunge maarufu kama kamati ya Mwakyembe kuwa tuhuma zile ni za kweli na kusababisha aliyekuwa Waziri
Mkuu,Edward Lowasa na Mawaziri wawili kujiuzulu hatimaye Rais kuvunja Baraza la Mawaziri.
Mafunzo hayo yamejumuisha wanahabari 28 kutoka mikoa minne ya Iringa, Mbeya, Rukwa na Ruvuma
Mwisho.
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Newer Post
Older Post
Home
0 comments:
Post a Comment
Thank you for reading the article
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Site search
Most Viewed
MBOZI METEORITE
THE MBOZI METEORITE By Kenneth Mwazembe Mob No. 0754 538920, 0762246322 Email : kmwazembe@yahoo.com , Kennethmwazembe@gmail.com Website: www...
Ugugaji kuku wa kienyeji
Ufugaji kuku na hasa wa kienyeji ndiyo njia pekee ya kumkomboa mwananchi vijijini kiuchumi. Serikali inapaswa kuhakikisha madawa ya mifugo ...
Mbozi meteorite a home for coffee plantation
Among of tourism attractions in Southern Highland region is Mbozi meteorite which is located about 70 km from Mbeya city. On the way to th...
MCHUNGAJI WA EAGT AFUNGWA JELA MIEZI 6
Mchungaji wa Kanisa la EAGT lillilopo mtaa wa Ichenjezya mjini Vwawa wilayani Mbozi mkoani Mbeya Simon Kitwike (48) jana alijikuta akihukumi...
Mgogoro wa Mashariki ya Kati (Middle East Crisis)
Levi Eshkol, David Ben-Gurion na Golder Meir hao wote ni mawaziri wakuu wa zamani wa Israel. Tangu Disemba 27 hadi 18 Januari 2009 vyombo vy...
WAFA WAKICHIMBUA VITO VYA WAJERUMANI
Mbozi September 27, 2008 VIFO WATU watatu wamefariki wakifukua hazina inayodhaniwa kufukiwa na wamishionari Wajerumani katika kijiji cha...
Simbeye azikwa
Buriani David Lumbala Simbeye Katika mazishi yake yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya baada ya mwili wa marehemu kuagw...
CAMARTEC kujenga mitambo ya Biogas 12000 nchini
Jinsi Camartec ilivyo jizatiti kuokoa misitu kwa kusambaza teknolojia ya matumizi ya gesi itokanayo na wanyama • CARMARTEC yatua Mbozi • ...
UCHELEWESHAJI WA PEMBEJEO KUWAATHIRI WAKULIMA WA MAHINDI WA WILAYA ZA MBOZI NA MOMBA
Wadaiwa shilingi 50,000 kwa ajili ya maabara za shule ndipo maombi yafikiriwe Serikali inahusika na kuwacheleweshea wakuli...
WANAFUNZI WATALII
Ziara ya wanafunzi wa shule ya awali na msingi ya Uwata Mbeya katika picha Mkuu wa kituo cha utafiti wa kahawa (Tacri) kituo cha Mbimba M...
Recent Posts
Text Widget
Copyright © 2012
Maisha ni Vita
| Powered by
Blogger
Design by
Web2feel
| Blogger Template by
NewBloggerThemes.com
Subscribe to Posts
|
Subscribe to Comments
0 comments:
Post a Comment
Thank you for reading the article