Thursday, May 30, 2013

Kilimo Kwanza

Posted by Unknown On 8:38 AM No comments
Sera au kauli mbiu ya kilimo kwanza imepokelewa na wananchi vijijini kwa matumaini makubwa lakini kwa bahati mbaya haijaeleweka ama kwa waenezaji wa sera hii kutoielewesha vilivyo kwa wakulima au utekelezaji wake umekuwa wa kisiasa zaidi. Ni katika kipindi hiki tumejionea pembejeo feki zikiuzwa kwa wakulima ikiwepo mbolea, madawa na mbegu. Matokeo yake tumeyashuhudia yaani janga la njaa kuikabili nchi yetu. pamoja na hayo taasisi husika zilijaribu kufuatilia hujuma hiyo ambapo maeneo mbalimbali walinaswa wachakachuaji hao na wengine kutoroka. Rushwa limeuwa suala kuu katika kuwashughulikia watuhumiwa hao, makampuni husika walijieleza vizuri wakiwa wamevaa mashati ya mikono mirefu mambo yamekwisha. Serikali ilianzisha MKUKUTA NA MKURABITA kwa nia njema lakini cha kushangaza Hakimiliki za kimila (Customary Title Deeds) zilizotarajiwa kuwasaidia wananchi vijijini zimekuwa kiini macho tu kwani mabenki au taasisi za fedha hadi Benki ya Rasilimali (TIB) wamezikataa kwa madai kuwa hazitambuliwi. Mimi ni mhanga wa hati hizi. Najiuliza; hivi hii serikali imepitisha sheria ya Ardhi ya vijiji No 5 ya mwaka 1999 kwa maigizo? Wilaya kama Mbozi huku niishiko sheria hiyo hiyo imekataza kutoa hati kubwa zinazotolewa na serikali yaani Wizara ya Ardhi je hii ni namna ya kutueleza uzuri wa kilimo kwanza? Nawapongeza Mfuko wa Pembejeo wa Taifa chini ya Mkurugenzi Mkuu Mariam Nkumbi kwa kuzitambua hati hizi na hivyo kuendelea kutoa mikopo kwa hati hizo. Hapa chini ni matokeo ya mchango wa Mfuko huo hapa Momba wilaya mpya.

0 comments:

Post a Comment

Thank you for reading the article

Site search

    More Text