Tuesday, December 30, 2008

MTOTO ANAYEHITAJI MSAADA WA KI-UTU

Posted by Unknown On 9:49 PM No comments


Mtoto Erica Laurent (1) aliyezaliwa bila njia ya haja kubwa amekuwa na tatizo la kufumuka nyuzi kila anaposhonwa katika hospitali ya rufaa Mbeya alipofanyiwa operation Novemba 2007. Baba wa mtoto Laurence Msongole amekataa kutoa fedha za matibabu, amemtelekeza mke baada ya kuzaa mtoto mwenye matatizo.

Hivi sasa mama wa mtoto Huruma Mwaijande anaishi kwa wazazi wake ambao nao wameshindwa kupata fedha za matibabu kufuatia umaskini unaoikabili familia hiyo.

Mtoto huyo amepangiwa kwenda Muhimbili kwa matibabu zaidi lakini uwezekano hauopo kutokana na ukweli kwamba familia haina uwezo hata wa kugharamia matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mbeya.

“Tulifukuzwa katika nyumba tuliyopanga na mume wangu, tukahamia kwa mama mkwe ambaye amepanga chumba na sebule, baba na mama mkwe wanalala chumbani na mimi na mume wangu tunalala sebuleni hali iliyonifanya nihame nije kuishi kwa wazazi wangu” anasema Huruma.

Mama na mtoto huyo wanaishi mtaa wa Ilembo mjini Vwawa wilayani Mbozi, wamefika ofisi ya mkuu wa wilaya kuomba msaada, ofisi hiyo imetoa kibali ili mama huyo azunguke mitaani kuomba msaada kwa wasamaria apate fedha za kumpeleka mgonjwa Muhimbili Dar es Salaam.

Huruma anao watoto wawili, ambapo mkubwa ni Sabina Laurence (3) na Erica ambaye ni mgonjwa.

Baba ya wa mtoto Laurence Msongole alipohojiwa juu ya tuhuma za kumtelekeza mke, anasema yeye hajagoma kutoa fedha ila hana fedha hizo hata nauli ya kwenda rufaa jijini Mbeya anashindwa.
Babu wa mtoto huyo Hatson Mwaijande anasema imekuwa ni mzigo kwake kwani mkwe wake amemwachia gharama zote za kuzunguka na mtoto, hata chakula chao ni shida inabidi awasaidie kwa kuwapa mtaji wa kuuza maparachichi kwa ajili ya kujikimu.
"Mkwe wangu ni fundi uashi lakini hatoi fedha kwa ajili ya famila yake, hii inasikitisha sana" anasema kwa masikitiko Mwaijande
Mwisho.

Monday, December 29, 2008

MTOTO ANYWA SUMU YA PANYA

Posted by Unknown On 8:43 PM No comments



Mtoto Derick Denis (8) akiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mbozi mjini Vwawa baada ya kunywa sumu ya panya kufuatia wazazi wake kushindwa kumnunulia mavazi ya Krismas. Je, ni umaskini au ?

Monday, December 15, 2008

Posted by Unknown On 7:53 AM No comments
Hizo ndizo zana za uvuvi katika kijiji cha Ikomba ufukweni mwa ziwa Nyasa maarufu kama Matema Beach.




Kazi ya kupiga makasia hufunzwa kwa vijana tangu wangali wadogo. Kijana akifanya mazoezi ya kupiga makasia ufukweni mwa ziwa hilo


Kazi za ufinyanzi zimewafanya wenyeji wa ufukwe huo kuwa maarufu na kuwa chanzo kikubwa cha kipato.

Wanawake husaidia kazi za uvuvi kwa kuchambua dagaa na kuwakausha. Mwanamke huyo hapo chini akichambua dagaa ufukweni.


Kinachovutia zaidi mbali na ufukwe ulivyo bora na safi, ni safu ya milima ya Living Stone inavyopamba mandhari hayo ya Matema.



Kazi za wakazi wa ziwa Nyasa pamoja na uvuvi, pia ni watengenezaji wa vyungu. Kazi ambazo wamekuwa wakirithisha vizazi hadi vizazi

ZIARA YA MATEMA ILIVYOFANA

Posted by Unknown On 7:37 AM No comments







Katika ziara hiyo tuliweza kujionea jinsi maanguko ya ardhi (Land slide) yalivyathiri maeneo mbalimbali kabla ya kufika Matema.

Mgahawa mzuri unaofaa kwa mahitaji ya utalii ulitoa huduma safi kwa waandishi waliofika eneo hilo. Hii ni nafasi ya waandishi kutangaza utalii na kutambulisha umma kwa vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Mbeya.
Gari hilo lililopambwa vema liliendeshwa na dreva mwanamke lilitufikisha salama licha ya matatizo madogo madogo ya njiani.
Tulijionea samaki wanaovuliwa ziwa Nyasa. Ziwa lilionekana kuwa na upungufu mkubwa wa samaki ambao ilielezwa kuwa tatizo linatokana na uvuvi usiozingatia utaalam.
Ziwa hilo linatoa samaki wa mapambo (wenye rangi) na ambao wakivuliwa husafirishwa nje ya nchi.








MATEMA BEACH -MBPC TOURS

Posted by Unknown On 7:12 AM No comments






The day when Mbeya Press Club members visited Matema Beach. It was a study tour whereas many journalists managed to explore many from this safari.

Site search

    More Text